• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa tisa wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na nchi za kiarabu wafanyika

    (GMT+08:00) 2020-07-07 18:47:23

    Mkutano wa tisa wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na nchi za kiarabu ulifanyika jana kwa njia ya video.

    Kwenye mkutano huo pande mbili za China na Nchi za kiarabu zilibadilishana maoni kwa kina kuhusu uhusiano wa kimkakati na kiwenzi, kujenga Jumuiya ya Mustakabali wa Pamoja kati ya China na nchi za kiarabu, na kufikia maafikiano.

    Taarifa ya pamoja kuhusu kupambana na COVID-19 iliyotolewa kwenye mkutano huo, imesema pande hizo mbili zinasisitiza kuimarisha mshikamano, kuhimiza ushirikiano na kusaidiana ili kupambana kwa pamoja na janga hili. Pia zimetoa wito kujenga jumuiya ya mustakabali wa pamoja kati ya China na nchi za kiarabu, na jumuiya ya afya kati ya pande hizo mbili. Katika Azimio la Amman lililotolewa kwenye mkutano huo, pande hizo mbili zimekubaliana kufanya mkutano wa viongozi na kuhusisha pendekezo la kujenga Jumuiya ya mustakabali wa pamoja kati ya China na nchi za kiarabu katika zama mpya. Mbali na hayo pande hizo mbili zimeweka mipango ya utekelezaji kati ya mwaka 2020 na 2022 ya Baraza la Ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako