• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China atoa mapendekezo matatu kuhusu kuhimiza uhusiano kati ya China na Marekani kwenye njia sahihi

    (GMT+08:00) 2020-07-09 17:10:57

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesisitiza kuwa China inapenda kukuza uhusiano na Marekani kwa kufuata moyo wa dhati, na kutoa mapendekezo ya kufungua njia zote za mazungumzo kati ya pande hizo mbili, na kuanzisha ushirikiano katika kupambana na virusi vya Corona.

    Bw. Wang Yi alisema hayo akihutubia Mkutano wa Baraza la vyombo vya habari la jopo la washauri bingwa kati ya China na Marekani lililofanyika kwa njia ya video. Bw. Wang ameeleza kuwa hivi sasa uhusiano kati ya China na Marekani unakabiliwa na changamoto kubwa zaidi tangu zianzishe uhusiano wa kibalozi kati yao. Baadhi ya wamarekani wanaichukulia China kuwa mshindani na hata adui kutokana na msimamo wenye upendeleo. Pia amesema kama uhusiano kati ya pande hizo mbili unaweza kurejea kwenye njia sahihi au la, hali hii itaathiri maslahi ya watu wa nchi hizo mbili, na pia mustakabali wa pamoja wa dunia na binadamu. Bw. Wang Yi anasema:

    "China haina nia ya kuzusha uchokozi au kuchukua nafasi ya Marekani, wala kuvutana kwa pande zote na Marekani. China inachukua msimamo wenye utulivu dhidi ya Marekani, na inapenda kuendeleza uhusiano na Marekani kwa kufuata moyo mwema na udhati. Ili kutimiza lengo hilo, pande hizo mbili zinapaswa kufanya juhudi za kusaidiana, kuheshimu sheria na kanuni za kimataifa, na kufanya mazungumzo kwa usawa."

    Bw. Wang Yi amesema katika miaka 40 iliyopita tangu uhusiano wa kibalozi kati ya China na Marekani uanzishwe, jumuiya ya maslahi ya pamoja kati ya pande hizo mbili imeundwa. Pande hizo mbili zinatakiwa kuchukua maendeleo ya uhusiano kati ya China na Marekani kwa mtizamo sahihi, na kushikilia njia ya kufanya mazungumzo na ushirikiano. Pia ametoa mapendekezo matatu kuhusu kuhimiza uhusiano kati ya China na Marekani kurejea kwenye hali ya kawaida. Anasema:

    "Moja ni kufungua njia zote za kufanya mazungumzo. China imefungua mlango wa kufanya mazungumzo, na iko tayari kurejesha mazungumzo ya ngazi mbalimbali na sekta mbalimbali. Pili, kukagua na kuorodhesha mazungumzo yatakayofanyika, ili kuthibitisha miradi ya ushirikiano utakaofanyika kati ya pande hizo mbili katika mambo ya pande hizo mbili na ya dunia nzima, na kuthibitisha masuala yenye migongano kati ya pande hizo mbili lakini yataweza kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo, pia kudhibiti matatizo ambayo ni vigumu kufikiwa maafikiano kati ya pande hizo mbili. Pendekezo la tatu ni kufuatilia na kuanzisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona."

    Kutokana na changamoto za maambukizi ya virusi vya Corona zinazoikabili dunia nzima, Bw. Wang Yi amesisitiza kuwa China inapenda kupeana habari kuhusu kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi, na uzoefu uliopatikana katika kupambana na virusi hivyo, na kuanzisha mawasiliano ya kina katika uwekaji wa mipango ya matibabu na utafiti wa chanjo ya virusi, na kwamba Marekani inatakiwa kuacha kuyahusisha mapambano dhidi ya virusi vya Corona na mambo ya kisiasa, kushirikiana na China katika mapambano dhidi ya virusi hivyo, na kubeba wajibu wake kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako