• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China: kutafuta chanzo cha virusi ni suala gumu la kisayansi

    (GMT+08:00) 2020-07-09 19:46:34

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo amesema, habari husika kutoka gazeti la Uingereza The Daily Telegraph imethibitisha tena kwamba kutafuta chanzo cha virusi ni suala gumu la kisayansi, kunapaswa kushirikisha wanasayansi kufanya utafiti wa kisayansi wa kimataifa katika dunia nzima.

    Bw. Zhao amesema ofisa wa WHO aliwahi kusema kutafuta chanzo cha virusi ni mchakato mrefu, huenda utahusisha nchi mbalimbali na sehemu mbalimbali. Inapswa kuwa na msimamo wazi kuhusu uwezekano wa aina mbalimbali wa chanzo cha virusi.

    Ameongeza kuwa China itaendelea kuunga mkono wanasayansi wa nchi mbalimbali kufanya utafiti kuhusu chanzo cha virusi na njia za maambukizi, na kuunga mkono nchi wanachama wa WHO kufanya ushirikiano kuhusu chanzo cha virusi katika wanayama.

    Hivi karibuni habari kutoka The Daily Telegraph inasema mtaalamu wa Chuo kikuu cha Oxford anaona virusi vya Corona havikutoka China, huenda vinaenea katika sehemu mbalimbali duniani, na vitaamka wakati mazingira yakivifaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako