• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazindua jukwaa la kimataifa la utafiti wa Akili Bandia

    (GMT+08:00) 2020-07-13 17:11:37

    China imezindua jukwaa la kitabibu la utafiti wa Akili Bandia (AI) wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Huduma za Afya kwa kutumia Akili Bandia uliofanyika Shanghai.

    Jukwaa hilo MedNet lilipendekezwa na Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) cha China (CAICT) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Jiao Tong cha Shanghai kwa lengo la kuendeleza utafiti na uvumbuzi katika teknolojia ya huduma ya afya kwa kutumia akili bandia na ushirikiano wa kimataifa katika utafiti.

    Mkuu wa CAICT Liu Duo amesema, MedNet italenga kufanya utafiti wa matumizi ya teknolojia ya akili bandia katika tiba ya dawa na afya ya umma. Pia amesema, jukwaa hilo litafuata mwongozo na uratibu kutoka Shirika la Afya Duniani, Umoja wa Mawasiliano ya Simu Duniani, na mashirika mengine ya kimataifa pamoja na vyuo vikuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako