• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalam wa WHO wawasili China kwa ushirikiano kuhusu utafiti wa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-07-13 20:52:03

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hua Chunying amesema, wataalam wawili wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wamefika nchini China kubadilishana maoni na wenzao wa China juu ya ushirikiano wa kisayansi katika kutafiti chanzo cha virusi vya Corona.

    Hua amesisitiza kuwa, maoni ya pamoja ya China na WHO ni kwamba, chanzo cha virusi hivyo ni suala la kisayansi ambalo linapaswa kufanyiwa utafiti na wanasayansi kupitia ushirikiano wa kimataifa. Pia WHO inaona kuwa huu ni mchakato utakaohusisha nchi na sehemu nyingi, na kwamba itatuma watalaam kwa nchi nyingine zinazowahitaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako