• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pengo kati ya matajiri na maskini laongeza hali ya wasiwasi ya haki za binadamu nchini Marekani

    (GMT+08:00) 2020-07-14 11:03:09

    Taasisi ya Utafiti wa Haki za Binadamu ya China imetoa makala kuhusu "pengo kati ya matajiri na maskini laongeza hali ya wasiwasi wa suala la haki za binadamu nchini Marekani".

    Makala hiyo imedhihirisha kuwa watu wenye kiwango cha mapato ya chini na ya juu wanashika nafasi kubwa zaidi nchini Marekani, tabaka la kati inaendelea kupungua, na kiwango cha umaskini kinaendelea kuwa juu. Mtoaji wa ripoti wa Umoja wa Mataifa kuhusu umaskini uliokithiri na haki za binadamu Bw. Philip Allston, amesema kwenye ripoti yake iliyotolewa mwezi Mei mwaka 2018 kuwa Marekani imekuwa nchi yenye pengo kubwa zaidi kati ya matajiri na maskini kati ya nchi za magharibi, na wamarekani milioni 4 wanaishi katika hali duni, na milioni 18.5 wakiwa kwenye umaskini uliokithiri.

    Makala hiyo imeeleza kuwa pengo kubwa kati ya matajiri na maskini nchini Marekani limeleta athari mbaya kwa haki za binadamu: karibu nusu ya familia za Marekani zinashindwa kuishi maisha ya kawaida, na watu wenye mapato ya chini wanakabiliwa na tishio la njaa, na kukosa fursa zenye usawa za elimu. Utafiti umeonesha kuwa, idadi ya watu wasio na makazi inaweza kuongezeka kwa asilimia 45 ndani ya mwaka mmoja kutokana na janga la virusi vya Corona, na kusababisha kuongezeka kwa msukosuko wa afya ya umma. Mbali na hayo maisha ya watu yamepungua huku kiwango cha watu kujiua kikiongezeka.

    Makala hiyo pia imesema, serikali ya Marekani inakosa nia ya kisiasa ya kupunguza pengo hilo, kwa kuwa mfumo wa kisiasa wa Marekani unahusiana kwa ukaribu na maslahi ya fedha yanayowakilishwa na serikali ya Marekani.

    Makala inaona pengo kubwa kati ya matajiri na maskini litadumishwa kwa muda mrefu nchini Marekani, na halitazamiwi kubadilishwa ndani ya muda mfupi, na athari mbaya zinazoletwa na hali hiyo dhidi ya umiliki na utimizaji wa haki za binadamu za wamarekani pia zitazidi kuwa baya siku hadi siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako