• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani iache kuchochea mgogoro katika suala la Bahari ya Kusini

    (GMT+08:00) 2020-07-14 19:35:17

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Zhao Lijian amesema, China inaitaka Marekani iache kuchochea mgogoro katika suala la Bahari ya Kusini.

    Kauli hiyo imekuja baada ya Wizara ya mambo ya nje ya Marekani kutoa taarifa jana kuwa,,matakwa mengi ya China katika suala la Bahari ya Kusini hayana msingi wa sheria za kimataifa, na kuzitaka nchi husika kupinga matakwa hayo.

    Zhao amesema, Marekani inapuuza historia na hali halisi ya Bahari ya Kusini, na kwenda kinyume na ahadi yake ya kutounga mkono upande wowote, imekiuka na kupotosha sheria za kimataifa kwa kuchochea mgogoro wa ardhi na bahari, kitendo ambacho kitaharibu amani na utulivu wa kikanda.

    Zhao amesisitiza kuwa China imetawala visiwa vya Bahari ya Kusini kwa zaidi ya miaka 1,000, na ilitangaza mstari wa mpaka wa bahari hiyo mwaka 1948, ambao haukupingwa na nchi yoyote kwa muda mrefu. Ameongeza kuwa China itaendelea kulinda mamlaka na usalama wake, na kushirikiana vizuri na nchi za kikanda kwa ajili ya kulinda amani na utulivu kwenye Bahari ya Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako