• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi na wataalamu wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini watoa wito kuimarisha ushirikiano kwenye mapambano dhidi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-07-15 17:55:37

    Jukwaa kuhusu ushirikiano kati ya China na Mashariki ya Kati katika mapambano dhidi ya janga la virusi vya Corona limefanyika hivi karibuni mjini Beijing. Viongozi wa kisiasa na wataalamu 19 kutoka nchi nane za Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini wamejadiliana na wasomi na wataalamu 29 wa China kupitia mtandao wa Internet kuhusu ushirikiano na mustakbali wa uhusiano kati ya China na nchi za Mashariki ya Kati. Washiriki hao wamesema kwa kauli moja kuwa janga la COVID-19 ni changamoto inayowakabili binadamu wote, na China na nchi za Mashariki zenye hatma ya pamoja zinapaswa kuungana mikono na kuimarisha ushirikiano.

    Akihutubia jukwaa hilo, Mkuu wa Akademia ya Sayansi Jamii ya China Bw. Xie Fuzhan amesema, China na nchi za kiarabu zinapaswa kuungana mikono na kuweka mfano wa kuigwa katika ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. Amesisitiza kuwa, mlipuko wa virusi vya Corona ulioibuka ghafla umewafanya watu wa nchi mbalimbali wajihisi kuwa binadamu wote wana hatma ya pamoja, na ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na janga hilo ndio chaguo sahihi.

    Chansela wa Chuo kikuu cha Sharjah cha Umoja wa Falme za Kiarabu Dk. Humaid Mjol Al Nuaimi amesema kwenye hotuba yake kuwa, mfumo wa kisiasa wa China umeonesha nguvu yake bora wakati wa kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona, na ushirikiano wa karibu kati ya China na nchi za kiarabu kwenye mapambano hayo umethibitisha urafiki imara kati ya pande hizo mbili.

    Aliyekuwa balozi wa Palestina nchini China Mustafa Al-Safarini amesema uhusiano kati ya China na nchi za kiarabu uko kwenye kipindi kizuri zaidi katika historia, na kwamba China kutoa taarifa kwa wakati kuhusu mlipuko wa COVID-19 na kuchangia uzoefu wake wa kupambana na ugonjwa huo, kumetoa nafasi na muda kwa nchi mbalimbali kujiandaa dhidi ya janga hilo, hatua ambazo zimefafanua kivitendo dhana ya Jumuiya ya Binadamu yenye Hatima ya Pamoja.

    Akizungumza kwenye jukwaa hilo, Mkuu wa Taasisi ya utafiti wa Uislamu ya Mfalme Faisal nchini Saudi Arabia Turki Al-Faisal ameeleza matarajio ya kusukuma mbele zaidi ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kusema kuwa miradi mbalimbali chini ya ushirikiano huo inaweza kutoa nafasi nyingi za ajira na kuhimiza maendeleo ya uchumi.

    Naye waziri mkuu wa zamani wa Misri Bw. Essam Sharaf amesema, ustaarabu wa China na Uarabu una mambo mengi yanayofanana, pande hizo mbili zinapaswa kuimarisha ushirikiano na mawasiliano, kutumia vizuri fursa ya ujenzi wa"Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kuufanya kuwa nyenzo muhimu ya kuhimiza ushirikiano wa kimataifa.

    Sawa na alivyosema waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi katika mkutano wa tisa wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na nchi za Kiarabu kuwa, hatma na mustakbali wa nchi mbalimbali vimeunganishwa kwa karibu, na baada ya kushinda mapambano ya pamoja dhidi ya janga hilo la virusi vya Corona, uhusiano kati ya China na nchi za kiarabu utakuwa umeimarishwa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako