• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yailaani Marekani kuzitishia nchi nyingine zisitumie Huawei

    (GMT+08:00) 2020-07-15 19:28:11

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hua Chunying leo kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema, rais Donald Trump wa Marekani anazilazimisha nchi nyingine zisitumie vifaa vya Kampuni ya Huawei ya China, kitendo ambacho kinathibitisha kuwa uamuzi wa kupiga marufuku matumizi ya vifaa vya Huawei hauna uhusiano na usalama, bali ni mchezo wa siasa.

    Hua amesema kitendo hicho pia kimetambulisha tena watu kuwa, nchi inayotishia, kuchokoza na kulazimisha nyingine si China, bali ni Marekani.

    Kauli hiyo imekuja baada ya rais Trump kukiri kuwa, amezishawishi nchi nyingi kuwa kama zinataka kufanya biashara na Marekani zisitumie vifaa vya Huawei, ama sivyo uhusiano kati yao na Marekani utaathiriwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako