• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idara ya Takwimu ya Taifa: Uchumi wa China unatarajiwa kufufuka katika nusu ya pili ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2020-07-16 18:22:18

    Msemaji wa Idara ya Takwimu ya Taifa ya China Bi. Liu Aihua leo amekutana na wanahabari na kusema, kutokana na mwelekeo mzuri wa hali ya kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya Corona, China imeharakisha hatua za kurejesha shughuli za kibiashara na uzalishaji mali, na uchumi wa China unatarajiwa kufufuka katika nusu ya pili ya mwaka huu.

    Takwimu zilizotolewa leo na Idara ya Takwimu ya Taifa ya China zinaonesha kuwa, Pato la Ndani la Taifa (GDP) katika nusu ya kwanza ya mwaka huu lilifikia yuan trilioni 45.66, ikiwa ni sawa na dola za kimarekani trilioni 6.52, ambayo imeshuka kwa asilimia 1.6 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho. Msemaji wa Idara ya Takwimu ya China Bi. Liu Aihua amesema, uchumi wa China ulianza kukua kuanzia robo ya pili ya mwaka huu.

    "Katika robo ya pili ya mwaka huu, pato la ndani la taifa liliongezeka kwa asilimia 3.2 kuliko mwaka jana kipindi kama hicho, na kuanza kukua baada ya kushuka kwa asilimia 6.8 katika robo ya kwanza ya mwaka, na vigezo vikuu vinaonesha kuwa uchumi umeboreka kidhahiri kuanzia robo ya pili ya mwaka."

    Msemaji huyo amesema, ukuaji huo haukupatikana kwa urahisi wakati China ilipokuwa inakabiliwa na changamoto kubwa ya janga la COVID-19 na mazingira ya kutatanisha ya ndani na nje ya nchi.

    Takwimu zinaonesha kuwa, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, watu milioni 5.64 mijini wamepata ajira, idadi ambayo imefikia asilimia 62.7 ya lengo la mwaka mzima. Bi. Liu Aihua amesema, serikali imeweka sera madhubuti za kuhimiza ajira na kuhakikisha maisha ya wananchi, ambazo zimeonesha ufanisi katika nusu ya kwanza ya mwaka huu.

    "Katika miezi ya karibuni kiwango cha ukosefu wa ajira mijini kimeendelea kupungua, na kufikia asilimia 5.7 mwezi Juni. Idadi ya watu wenye ajira ambao hawakuenda kazini katika kipindi cha COVID-19 pia imeendelea kushuka na kufikia asilimia 0.8 hadi kufikia mwezi Juni, ikiwa ni sawa na mwaka jana. Kwa hivyo, kutokana na sera za kuhimiza ajira, mabadiliko chanya kwa hali ya ajira yameonekana tangu nusu ya kwanza ya mwaka huu."

    Aidha, takwimu pia zinaonesha kuwa katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, sekta ya viwanda ya China imerejesha uzalishaji hatua kwa hatua, mauzo ya mtandaoni yameongezeka kwa kasi, na muundo wa biashara ya nje umeendelea kuboreka. Mtafiti wa Ofisi ya Makonsela ya Baraza la Serikali la China Bw. Yao Jingyuan anaona kuwa, uchumi wa China utadumisha mwelekeo wa kufufuka katika nusu ya pili ya mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako