Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hua Chunying amesema, serikali ya Uingereza imekosa uhuru na kujiamulia katika suala la Huawei, na uamuzi wake wa kupiga marufuku Huawei utaleta hasara kwake.
Kauli hiyo imekuja baada ya ikulu ya Uingereza kukiri kuwa sababu ya Uingereza kubadilisha msimamo wake kuhusu Huawei ni Marekani kutishia kuiwekea Uingerza vikwazo.
Hua amesema katika miaka 20 iliyopita, ushirikiano mzuri kati ya Huawei na Uingereza unalingana maslahi ya nchi hiyo, na Uingereza utajidhuru kutokana na uamuzi wake wa kupiga marufuku vifaa vya Huawei kwenye ujenzi wake wa vituo vya 5G.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |