• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: PEP yafunga maduka yake nchini Uganda

  (GMT+08:00) 2020-07-20 15:41:27

  Kufikia mwisho wa mwaka huu, maduka ya PEP, yanayoongoza kwa kuuza nguo kwa bei nafuu barani Afrika, yatafunga maduka yake yote nchini Uganda. Zaidi ya wafanyikazi 80 watapoteza ajira zao.

  Mojawapo ya sababu kuu ya kufingwa kwa maduka hayo nchini Uganda ni shinikizo linalotokana na janga la virusi vya corona.

  Meneja mkuu wa PEP nchini Uganda bwana Liaan Max Scholtes, alithibitisha taarifa hii alipohojiwa na gazeti kuu nchini Uganda. Bwana Max lidokeza kuwa sababu nyingine ya kufungwa kwa maduka hayo ni ushindani mkali uliopo kwa sasa kwa sababu ya athari za virusi vya corona.

  Kuna maduka 13 ya PEP nchini Uganda na eneo moja la usambazaji. PEP ina jumal ya maduka 300 katika mataifa saba barani Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako