• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania katika miaka mitatu ijayo itakuwa mzalishaji mkubwa wa umeme na msambazaji katika eneo la Afrika Mashariki

  (GMT+08:00) 2020-07-21 20:02:08

  Tanzania katika miaka mitatu ijayo itakuwa mzalishaji mkubwa wa umeme na msambazaji katika eneo la Afrika Mashariki kufuatia serikali ya awamu ya tano kwa ujasiri kutekeleza mpango wa Julius Nyerere Hydropower kando ya Mto Rufiji katika Mkoa wa Pwani.

  Mradi wa ukuzaji umeme wa mkubwa ambao unafadhiliwa na serikali kwa gharama ya 6.55tri ulianza Juni mwaka jana na unatarajiwa kukamilika katika miaka miwili ijayo.

  Mradi wa umeme wa megawatits 2,115 utakuwa bwawa la nne kubwa barani Afrika na la tisa ulimwenguni.

  Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amesema hivi karibuni kuwa serikali tayari imelipa 1.19tri.

  Mradi wa umeme wa Julius Nyerere unatarajia kubadilisha sekta ya nishati na kuihakikishia nchi kuwa na nguvu ya umeme ya kutosha na kuongeza kasi ya maendeleo ya Sekta zingine za kiuchumi sanasana ukuaji wa uchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako