• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AMINA MOHAMMED AUNGWA MKONO NA BARAZA LA BIASHARA LA AFRIKA MASHARIKI KUWANIA KITI CHA WTO

    (GMT+08:00) 2020-07-27 15:40:30

    Katika historia yake, Shirik la Biashara Ullimwenguni halijawahi kuw ana mkurugenzi mkuu kutoka bara la Afrika. Ila, endapo dalili zilizopo zitazaa matunda, basi waziri wa Michezo wa Kenya, Amina Mohammed atakuwa mwanamke wa kwanza na mwafrika wa pekee kuwahi kuongoza shirika la biashara ulimwenguni katika nafasi ya mkurugenzi mkuu.

    Tayari baraza la biahsara la Afrika Mashariki limetangaza kumuunga mkono Amina, ambaye anapata upinzani kutoka kwa wagombea wengine saba, wanaotoka mataifa mbali mbali ulimwenguni.

    Afrika ina wagombea watatu wa kiti hicho ambao ni Amina Mohammed kutoka Kenya, Ngozi Okonjo-Iweala wa Nigeria na Abdel-Hamid Mamdouh kutoka Misri.

    Kinachompa Amina nafasi nzuri ya kutwaa kiti hiki ni uzoefu wake katika maswala ya kibiashara ya kimataifa. Amina amewahi kuwa mwenyekiti wa baraza la kimataifa la kuhakiki sera za biashara duniani. Bi Amina Mohammed pia alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa kumi wa mawaziri wa Shirika la bishara ulimwenguni mwaka wa 2015, jijini Nairobi.

    Kando na uzoefu huu wa kufanya kazi na shirika hili la biashara ulimwenguni, Amina vile vile amewahi kuwa balozi wa Kenya na ana uhusiano mzuri wa kidiplomasia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako