• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya Wakulima wa pamba Yatta wapokea Sh2 milioni

  (GMT+08:00) 2020-07-28 19:12:35

  WAKULIMA wa pamba eneo la Yatta, Kaunti ya Machakos, wanajivunia kupata mavuno ya juu msimu huu.

  Wakulima hao wana jambo la kujivunia baada ya kampuni ya Thika Cloth Mills Ltd kununua pamba yote waliovuna.

  Mwaka 2019 wakulima hao walianza kufanya kilimo cha pamba kinyume na hapo awali ambapo eneo hilo lilikuwa kavu bila kupandwa chochote.

  kampuni ya Thika Cloth Mills iliyowahimiza wakuze mipamba kupata pamba. Ilifanya hivyo kwa kuwapa mbegu, mbolea, na dawa za kunyunyuzia ili kuboresha ukulima wao.

  Katika muda wa wiki moja iliyopita, kampuni hiyo ilipiga kambi katika maeneo ya Yatta, na Ndalani ambapo ilinunua pamba kutoka kwa wakulima zaidi ya 100 ambapo iliwalipa takribani Sh2 milioni kwa mavuno ya pamba.

  wakazi wa Yatta wamepongeza serikali kwa kukubalia wakazi hao kupanda pamba ambayo imeweza kunawiri.

  Meneja mkuu wa kampuni ya Thika Cloth Mills Ltd, Bw Dickson Kariuki amesema kampuni hiyo ina uwezo wa kupokea hadi tani 10,000 kutoka kwa wakulima hao katika kaunti nzima ya Machakos.

  Amesema tayari wameingia katika mkataba na wakulima wa Kaunti ya Lamu, Meru, Homa Bay, Kisumu na Siaya ili wanunue pamba kutoka maeneo hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako