• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapenda kusukuma mbele mazungumzo na nchi za ASEAN kuhusu "Kanuni ya Mienendo katika Bahari ya Kusini"

    (GMT+08:00) 2020-07-28 20:55:11

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema, China inapenda kushirikiana na nchi wanachama wa Umoja wa Nchi za Asia ya Kusini-Mashariki ASEAN, kusukuma mbele mazungumzo kuhusu "Kanuni ya Mienendo katika Bahari ya Kusini", ili kufikia mwafaka na nchi hizo mapema iwezavyo.

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo hivi karibuni amesema, Bahari ya Kusini si "eneo la kibeberu la China baharini", na China imekiuka sheria ya kimataifa. Bw. Wang amesema watu wote wanajua Marekani inatafuta maslahi yake kwa kisingizio cha kulinda sheria ya kimataifa, na inajaribu kuchochea mgogoro katika Bahari ya Kusini.

    Bw. Wang amesisitiza kuwa sera ya China kuhusu Bahari ya Kusini ni endelevu na haibadiliki, China hutekeleza kwa makini sheria za kimataifa ikiwemo Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Sheria ya Bahari (UNCLOS), haikuwahi kuongeza matakwa ya eneo, na siku zote inashikilia kutatua migogoro ya ardhi na bahari na nchi jirani kwa njia ya mazungumzo, kwa mujibu wa sheria ya kimataifa na kwenye msingi wa kuheshimu ukweli na historia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako