• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wang Yi asema China kitajibu kithabiti dhidi ya Marekani

    (GMT+08:00) 2020-07-29 09:35:31

    Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana aliongea na mwenzake wa Ufaransa kwa njia ya simu, na kueleza maoni yake juu ya uhusiano kati ya China na Marekani.

    Bw. Wang Yi amesema, hivi karibuni uhusiano kati ya pande mbili umeleta wasiwasi kwa jumuiya ya kimataifa, na sababu ya kimsingi ni kwamba baadhi ya nguvu za kisiasa nchini Marekani zinatokana na mahitaji ya kisiasa kwenye kampeni ya uchaguzi na kulinda hali ya umwamba ya upande mmoja, pia zinaikana historia ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, kupambana na China kwa pande zote bila msingi wowote, kuchochea maslahi ya kiini cha China, na kushambulia utaratibu wa kijamii unaochaguliwa na watu wa China.

    Bw. Wang Yi amesema, China itajibu kithabiti na kwa njia za kimantiki dhidi ya Marekani. Ambapo kwanza, China itajibu hatua za Marekani za kuharibu maslahi halali ya China. Pili, China na Marekani zinapaswa kuwasiliana kwa usawa, kulinda utulivu wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Tatu, jumuiya ya kimataifa inapaswa kulinda mshikamano na ushirikiano kwa pamoja. Aidha nchi mbalimbali zinapaswa kushirikiana kupinga hali ya upande mmoja na umwamba, na kulinda hali ya jumla ya amani na maendeleo duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako