• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa kipaumbele kwa maslahi ya umma kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-07-29 17:23:28

    Baada ya kuibuka kwa mlipuko wa virusi vya Corona, ambao ni dharura kubwa zaidi ya afya ya umma kutokea nchini China tangu China mpya ilipoanzishwa mwaka 1949, serikali kuu ya China, ikiwa chini ya uongozi thabiti wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China yenye Rais Xi Jinping kuwa kiini chake, imeshikilia kutoa kipaumbele kwa maslahi ya wananchi kwenye mapambano makubwa ya umma dhidi ya virusi hivyo, hali ambayo inaonesha dhana ya haki za binadamu inayotoa kipaumbele kwa maslahi ya watu.

    Kwenye mapambano ya umma dhidi ya virusi vya Corona, China siku zote imeweka mkazo katika kulinda usalama wa maisha na afya ya wananchi, na kutekeleza kivitendo dhana ya haki za binadamu inayozingatia maslahi ya wananchi. Ili kuzuia kuenea zaidi kwa virusi, tarehe 23 mwezi Januari, Mji wa Wuhan wenye watu zaidi ya milioni kumi, ambao ni kitovu muhimu cha mawasiliano nchini China tangu kale, ulisitisha huduma zote za usafiri wa umma, ikiwemo usafiri wa mabasi, Subway, vivuko, treni na ndege. Uchunguzi uliofanywa na taasisi 15 maarufu za utafiti duniani, umeonesha kuwa kufungwa kwa mji wa Wuhan kumekuwa ni tukio kubwa zaidi la karantini katika historia ya binadamu, hatua ambayo ilisaidia kupunguza maambukizi kwa watu zaidi ya laki saba. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amebaini kuwa, watu wa China wametoa mchango kwa binadamu wote kwa "kujitoa muhanga wa kujibana maisha yao ya kawaida".

    Baada ya mji wa Wuhan kufungwa, mikoa yote na majeshi ya China walituma timu 346 za matibabu zenye madaktari na wauguzi 42,600 kwenda mkoani Hubei, na wanaakademia kumi wa magonjwa ya mlipuko wa China pia walishiriki katika mapambano hayo kwenye mstari wa mbele. China pia ilihamasisha raslimali zote bora kuuunga mkono mkoa wa Hubei, ili kulinda usalama na afya ya watu walioambukizwa virusi hivyo hatari.

    Kwenye vita hiyo dhidi ya virusi vya Corona, China imetilia maanani katika kuwajali na kuwatunza makundi ya watu dhaifu kwenye jamii. Katika mkutano uliofanyika Machi 6 kuhusu upunguzaji wa umaskini, serikali ya China imeahidi kutimiza lengo la kutokomeza umaskini vijijini mwaka huu kama ilivyopangwa, na pia kufikia lengo la kupunguza umaskini kwenye Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya 2030 mapema zaidi kwa miaka kumi.

    Baada ya janga la virusi vya Corona kuenea kote duniani, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Mei, China ilikuwa imetoa uzoefu na mipango ya kinga na tiba kwa nchi 180, na mashirika kumi ya kikanda na kimataifa kote duniani, ilituma timu za matibabu kwenda kwenye nchi zenye mahitaji ya dharura, na kutoa misaada ya vifaa tiba kwa nchi 150 na mashirika manne ya kimataifa.

    Kwenye mkutano wa afya duniani uliofanyika Mei 18 kwa njia ya mtandao, China iliahidi kuwa chanjo ya virusi vya Corona itakayotengenezwa na China itatolewa kama Bidhaa za Umma Duniani (Global Public Goods).

    China ikiwa ni nchi kubwa inayowajibika, itaendelea na juhudi zake za kulinda na kuhakikisha haki mbalimbali za wananchi, na kuendelea kusukuma mbele maendeleo yenye uwiano ya shughuli za haki za binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako