• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Magufuli aubadili jina uwanja wa Taifa na kuuita Mkapa Stadium

    (GMT+08:00) 2020-07-29 17:26:36

    RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli ameubadili jina Uwanja wa Taifa na sasa utakuwa unajulikana kama Uwanja wa Mkapa ili kumuenzi Rais mstaafu wa Serikali ya awamu ya tatu nchini, marehemu Dk. Benjamin William Mkapa. Mkapa aliyefariki dunia Julai 24 Jijini Dar es Salaam ndiye aliyefanikisha ujenzi wa Uwanja huo wa kisasa wa michezo nchini. Akizungumza wakati wa zoezi la kuuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Mkapa uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam leo, Rais Dk. Magufuli amesema amepokea ujumbe mwingi sana kutoka kwa wananchi kuhusu kubadilijina la uwanja huo. Amesema licha ya kuwa Mkapa mwenyewe hakupenda jina lake litumiwe namna hiyo, watanzania wanataka kumkumbuka kwa njia hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako