• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Yanga yamaliza usajili asilimia 90 kwa wachezaji wa ndani.

    (GMT+08:00) 2020-07-29 18:15:06

    Klabu ya Yanga ya Tanzania imesema imekamilisha asilimia 90 ya usajili wa wachezaji wa ndani na sasa iko kwenye mipango thabiti ya kuanza kusajili wachezaji wa kigeni. Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli amesema kwenye suala la usajili katika klabu hiyo hakuna shida kabisa, kwani mambo yameshaanza na yanakaribia kumalizika baada ya wiki moja au mbili hivi. Alisema wachezaji wote hao wamesajiliwa baada ya kupendekezwa na benchi la ufundi. Kwa sasa Yanga ina muda wa wiki moja au mbili hivi wa kukamilisha usajili wachezaji wa ndani, wale ambao benchi la ufundi waliopendekeza au kutafuta mbadala wao kama itashindikana kuwapata wote. Kocha msaidizi wa Yanga Boniface Mkwasa alijiweka pembeni taarifa za ndani zikidai kuwa alikuwa haelewani na Mbelgiji huyo, haijulikani kama amesimamia usajili huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako