• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa China asisitiza suala la Yemen litatuliwe kwa njia ya kisiasa

    (GMT+08:00) 2020-07-29 18:58:01

    Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun tarehe 28 kwenye mkutano wa baraza la usalama kuhusu suala la Yemen, ametoa taarifa akisisitiza suala la Yemen litatuliwe kwa njia ya kisiasa.

    Balozi Zhang Jun amesema hali ya sasa nchini Yemen si yenye matumaini, watu wamekuwa wakisumbuliwa na vita, njaa na maafa. Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuongeza juhudi kuhimiza suala la Yemen kutatuliwa kwa njia ya kisiasa haraka iwezekanavyo.

    Amesema, Kwanza pande zote zinazopambana zinapaswa kusimamisha vitendo vya kijeshi mara moja na kutuliza hali ya usalama. Pili inapaswa kushikilia mwelekeo wa utatuzi wa kisiasa na kuendelea kuhimiza usuluhishi. Tatu inapaswa kuboresha hali ya kibinadamu nchini Yemen na kuhakikisha misaada ya kibinadamu inaingia Yemen.

    Balozi Zhang Jun pia ameeleza kufuatilia suala la meli ya mafuta ya Sapphire na kutoa mwito kwa pande zote ziendelee na mazungumzo na kuhakikisha timu ya kiufundi ya Umoja wa Mataifa inaifanyia tathmini ya usalama na matengenezo meli hiyo haraka iwezekanavyo, ili kuepuka janga la kimazingira, kibinadamu na kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako