• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Afghanistan yaahidi kuachia huru wafungwa 600 wa Taliban

    (GMT+08:00) 2020-07-29 19:23:47

    Ikulu ya Afghanistan imetoa taarifa ikisema rais Ashraf Ghani wa nchi hiyo ameahidi kuwaachia huru wafungwa 600 wanaobaki wa Kundi la Taliban, ili kutoa mazingira kwa ajili ya mazungumzo ya ndani kati ya pande hizo mbili.

    Kuachiana wafungwa ni sehemu ya makubaliano ya amani yaliyofikiwa na Marekani na Taliban mwishoni mwa Februari mwaka huu. Mwanzoni mwa mwezi Machi, rais Ghani aliamuru kuachiwa kwa wafungwa 5,000 wa Taliban. Hadi kufikia sasa serikali ya Afghanistan imewaachia huru wafungwa takriban 4,400 wa Taliban, huku upande wa Taliban ukiwaachia huru zaidi ya askari 800 wa usalama wanaoshikiliwa. Tarehe 7 mwezi huu, serikali ya Afghanistan ilitangaza kusimamisha kuwaachia wafungwa waliobaki wa Taliban, ambao wanadaiwa kuwa na hatia mbaya.

    Habari nyingine zinasema Kundi la Taliban limetangaza kusitisha mapambano kati ya tarehe 31 Julai na tarehe 2 Agosti, wakati wa Eid al Adha. Uamuzi huu umekaribishwa na rais Ghani, akiamuru vikosi vya usalama vifuate makubaliano ya kusimamisha vita, isipokuwa kama vikishambuliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako