• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Wajasiriamali wapokea mafunzo kutoka kwa Shirika la Viwango

  (GMT+08:00) 2020-07-29 19:25:43

  Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendesha mafunzo maalumu ya ujasiriamali na umuhimu wa ubora wa bidhaa kwa wajasiriamali mkoani Kagera kwa lengo la kuboresha bidhaa zao na kuendana na ushindani katika soko la dunia.

  Mafunzo hayo yalifanyika jana katika ukumbi wa hoteli ya Bukoba yakiwashirikisha zaidi ya wajasiriamali 50 kutoka wilaya za mkoa huo.

  Akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawiro, alilishukuru shirika hilo kwa kuwafikia wajasiriamali kwenye maeneo yao na kuweza kuzijua changamoto zao katika usindikaji wa bidhaa zao.

  Kinawiro amesema kuwa wajasiriamali ni watu muhimu katika ukuaji wa uchumi wa taifa ambao wanatakiwa kusaidiwa kwa kupewa elimu ya ujasiriamali na utunzaji wa bidhaa tangu zikiwa malighafi hadi hatua ya kwenda sokoni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako