• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa WHO wafanya mawasiliano ya kina na wenzao wa China

    (GMT+08:00) 2020-07-30 09:57:53

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin jana alisema, wataalamu wawili wa WHO wamekuja China mwezi huu kufanya mazungumzo ya awali ya ushirikiano wa kutafuta chanzo cha virusi vya Corona.

    Wataalamu hao walifanya mkutano kwa njia ya video na wenzao wa China mara kwa mara wakati walipokuwa wamejitenga, ambapo wamefanya mawasiliano ya kina kuhusu maendeleo ya kazi za wadau wa sayansi duniani kutafuta chanzo na njia za usambazaji za virusi vya Corona, na mpango wa kazi za utafiti wa kisayansi katika kipindi kijacho.

    Bw. Wang Wenbin amesema, China na WHO zina maoni ya pamoja ya kimsingi, ambapo kutafuta chanzo ni suala la kisayansi, na inapaswa kuwapa wanasayansi fursa ya kufanya utafiti wa sayansi na ushirikiano wa kimataifa katika dunia nzima. Pia kazi ya kutafuta chanzo ni mchakato endelevu, huenda utahusiana na nchi mbalimbali na sehemu mbalimbali, WHO itafanya ukaguzi katika nchi nyngine kutokana na mahitaji yake. China inatumai nchi zote husika zitatoa ushirikiano kwaWHO kama China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako