• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AIIB yajitahidi kujijenga kuwa mfano mpya wa ushirikiano wa kimataifa kati ya pande nyingi

    (GMT+08:00) 2020-07-30 17:36:03

    Mkutano wa tano wa mwaka wa Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia AIIB ulifanyika kuanzia Jumanne hadi Jumatano wiki hii kwa njia ya video. Mkutano huo umesisitiza kuwa, AIIB itaendelea kutekeleza taratibu za pande nyingi, na kujitahidi kujijenga kuwa mfano mpya wa ushirikiano wa kimataifa kati ya pande nyingi.

    Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia yenye makao makuu mjini Beijing ilianzishwa rasmi Januari 16 mwaka 2016 kutokana na pendekezo la China. Hivi sasa idadi ya nchi wanachama wa benki hiyo imeongezeka kutoka 57 ya mwanzoni hadi nchi 103 kutoka mabara sita. Katika miaka minne iliyopita, AIIB imewekeza dola za kimarekani bilioni 20 kwenye miradi zaidi ya 80 ya miundombinu katika nchi 24 wanachama, uwekezaji ambao umehimiza muunganiko wa kikanda na mafungamano ya kiuchumi, na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Asia na dunia nzima.

    Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, mlipuko wa virusi vya Corona umetoa pigo kubwa kwa uchumi wa dunia. Ili kukabiliana na janga hilo na kuziunga mkono nchi wanachama kufufua uchumi, Benki ya AIIB imeweka mfuko wa dharura wa dola za kimarekani bilioni kumi. Hadi sasa, mfuko huo umetoa uungaji mkono wa kifedha wa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 5.9 kwa miradi mbalimbali katika nchi 12, zikiwemo India, Bangladesh na Thailand. Akizungumza kwenye mkutano huo, mkurugenzi mkuu wa AIIB Bw. Jin Liqun amesema, janga hilo la virusi vya Corona limefichua udhaifu wa nchi zenye kipato cha chini, haswa kwenye nyanja ya afya na matibabu, ambayo itakuwa moja ya sekta zitakazopewa kipaumbele na AIIB katika siku zijazo. Anasema:

    Sauti 1

    "Katika siku zijazo, bila kujali kama AIIB itarejea kwenye miradi ya jadi ya miundombinu kama vile ujenzi wa barabara, reli au bandari, au itaanza kugusa miradi ya maendeleo endelevu kama vile uchakataji wa maji taka, hakika tutatenga raslimali kiasi kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya afya na matibabu. Kwa kuwa sekta hiyo itaweza kuongeza ubora wa raslimali watu, na hata kuongeza tija kwa nchi. Miundombinu ya nyanja hii pia ni muhimu sana, hili pia ni somo tulilojifunza kutokana na janga la virusi vya Corona."

    Benki ya AIIB ni benki ya aina mpya ya maendeleo kati ya pande nyingi. Katika miaka minne iliyopita, imeshikilia kanuni za kufanya maamuzi kupitia majadiliano na kuhakikisha matunda ya maendeleo yananufaisha wote. Ushirikiano mzuri kati ya AIIB na taratibu nyingine za pande nyingi umefafanua wazi dhana ya pande nyingi. Bw. Jin Liqun amesema, mapambano ya pamoja dhidi ya virusi vya Corona kote duniani hayawezi kuondokana na ushirikiano wa pande nyingi.

    Sauti 2

    "Wakati janga la virusi vya Corona linaenea kote duniani, hakuna nchi yoyote inayoweza kuepuka na kujinurusu peke yake. Hii ndio ni sababu AIIB imeanzisha ushirikiano na Benki ya Maendeleo ya Asia na Benki ya Ujenzi na Maendeleo ya Ulaya, na kutoa vifaa tiba kwa nchi nyingi na kutoa uungaji mkono wa kifedha kwa sekta binafsi na serikali. Ingawa baadhi ya watu wanaona hatua hii haitafanya kazi, lakini kwa ukweli, huu ndio ni ufumbuzi wa changamoto zinazotukabili. Katika miezi minne hadi mitano iliyopita, kama hakuna uungaji mkono wa taratibu za pande nyingi, huwezi kukisia changamoto gani kubwa zitazikabili nchi zenye mapato ya chini."

    Mjumbe wa jopo la washauri wa kimataifa la AIIB Bibi Ngozi Okonjo-Iweala, ambaye aliwahi kuwa waziri wa fedha wa Nigeria na mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Dunia, anaona ni muhimu kwa AIIB kuendelea kutekeleza dhana ya pande nyingi, ili kuweza kukabiliana na changamoto mpya katika siku zijazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako