• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pluijm aahidi mazuri Yanga kama atapewa nafasi ya kurudi tena

    (GMT+08:00) 2020-07-30 18:46:05

    Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van der Pluijm, amezungumzia tetesi za kurejea nchini kuchukua mikoba ya kuifundisha timu hiyo iliyoachwa na Mbelgiji Luc Eymael aliyetimuliwa kutokana na lugha chafu za za kibaguzi. Pluijm ni mmoja wa makocha waliowahi kuiongoza Yanga kwa mafanikio, lakini aliondolewa na baadaye kwenda kufanya kazi Singida United ya Singida na Azam FC ya jijini Dar es Salaam. Akizungumza jana, Pluijm, alisema amesikitika kuona Yanga 'imepotea' tangu alipoondoka na endapo inataka kushinda mataji isifanye makosa katika kuchagua kocha mwingine atakayekiongoza kikosi cha timu yao. Pluijm alisema anaifahamu vema timu hiyo pamoja na soka la Tanzania, hivyo kwake hatakuwa na wakati mgumu katika kutekeleza majukumu yake endapo atarejea nchini kufanya kazi. "Ni juu yao, uamuzi ni wao, wao ndio wanajua wanataka klabu yao iende wapi, wanatakiwa kuwa makini kama wanataka mataji, hakuna kubahatisha.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako