• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hatma ya Fred Felix Minziro katika klabu ya Mbao FC njia panda

    (GMT+08:00) 2020-07-30 18:46:32

    Uongozi wa klabu ya Mbao FC inayopambana kujinusuru kubakia Ligi Kuu Tanzania Bara umesema hatima ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Fred Felix Minziro itajulikana baada ya kumalizika kwa mechi ya hatua ya mtoano itakayochezwa Jumamosi. Minziro aliiongoza vema Mbao FC iliyokuwa mkiani hadi kupata tiketi ya kucheza mechi za mtoano na endapo atashinda, timu hiyo itabakia kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara. Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa Mbao FC, Richard Melli, alisema walimpa Minziro timu hiyo kwa lengo la kuinusuru isishuke daraja, sasa bado wanasubiri kuona mwisho wa kazi waliyompatia., wakiwa na imani kuwa atafanikiwa kuwabakisha kutokana na kiwango walichokionyesha kwenye baadhi ya mechi za Ligi Kuu Bara zilizomalizika hivi karibuni. Amesema ni mapema kuweka wazi suala la yeye kuendelea kubaki kuifundisha timu hiyo. Amesema Mbao FC inaheshimu kazi na mchango aliotoa kocha huyo na kwa sasa wanaamini anaweza kuwasaidia wasishuke daraja ingawa wanafahamu haitakuwa kazi rahisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako