• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanadada wa Kenya Ingosi wa Harambee Starlets apania soka ya klabu ng'ambo

    (GMT+08:00) 2020-07-30 18:47:16

    Kiungo mkabaji wa Harambee Starlets, Ruth Ingosi, amefichua mipango yake ya msimu ujao katika kikosi cha FC Lakatamia nchini Cyprus. Ruth alisajiriwa rasmi ya Lakatamia mwanzoni mwa mwaka huu baada ya kuagana rasmi na klabu ya Eldoret Falcons. Alikosa fursa ya kuoanisha vilivyo mtindo wake mchezo wake na wa wanasoka wenzake kikosini baada ya kampeni za msimu kuvurugwa na janga la corona. Hadi Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake nchini Cyprus iliposimaishwa ghafla mnamo Machi 2020, zaidi ya robo tatu za mechi zilikuwa zimesakatwa. Ingosi aliwezeshwa kucheza mechi nne pekee iliyomshuhudia akifunga mabao mawili na kusaidia waajiri wake hao kukamata nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi wenye timu 12. Wanasoka wa FC Lakatamia wanatarajiwa kurejea kambini wiki ijayo kwa minajili ya kujifua kwa msimu mpya utakaoanza Septemba. Ingosi amesema katika maazimio yake ni kuonyesha uwezo wake kwa waajiri wake katika msimu wa 2020-21 kwa matumaini ya kukamilisha kampeni miongoni mwa vikosi viwili vya kwanza na kufuzu kwa soka ya bara Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako