• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Simba yaonekana kuwazidi ujanja Yanga kutaka kumsajili Makambo

    (GMT+08:00) 2020-07-30 18:47:35

    Klabu ya Simba imeingia kwenye mpango wa kuiwinda saini ya Heritier Makambo aliyewahi kuwa mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Heritier Makambo. Makambo aliachana na Yanga msimu wa 2017/18 akiwa ni mfungaji wa tatu kwenye ligi ya Tanzania akiwafuata Meddie Kagerena Salim Aiyee. Kwa sasa Makambo anaichezea Klabu ya Horoya AC ya nchini Guinea alisaini mkataba wa miaka mitatu kuichezea timu hiyo. Habari zinaeleza kuwa tayari uongozi wa Simba umeshaanza kufanya mazungumzo na mabosi wa Horoya ili kupata saini ya nyota huyo. Katika msimu ujao Yanga itapata tabu kwani idadi kubwa ya wachezaji wake wanaweza kuonekana wakiwa katika klabu Simba na mpaka sasa asilimia kubwa kwa Makambo kukipiga Simba msimu ujao. Yanga ilishindwa kuvunja mkataba wa Makambo na Horoya AC ila ndani ya Simba kila kitu kimekuwa sawa na bodi imekubali kufanikisha hilo. Taarifa za awali zilieleza kuwa Yanga ilikuwa inaiwinda saini ya nyota huyo ili arejee ndani ya kikosi hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako