• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump aongeza uwezekano wa kuchelewesha uchaguzi mwezi Novemba

    (GMT+08:00) 2020-07-31 09:15:26

    Rais wa Marekani Donald Trump ameongeza uwezekano wa kuchelewesha uchaguzi mwezi Novemba, akidai kwamba kupiga kura kwa njia ya sanduku la barua kutafanya uchaguzi wa mwaka 2020 uwe na majibu yasiyo sahihi na wa udanganyifu katika historia.

    Trump ameendelea kusema kwamba hatua hii itakuwa aibu kubwa kwa Marekani na kushauri kuchelewesha uchaguzi hadi watu waweze kupiga kura vizuri na kwa usalama.

    Seneta wa Marekani Tom Udall ambaye ni mwanachama wa Democratic kutoka New Mexico ameandika kwenye twitter yake kwamba Trump hawezi kuchelewesha uchaguzi na kwamba anajaribu kuwachanganya wananchi kutokana na kushughulikia vibaya janga la virusi vya corona. Naye seneta wa Republican Lindsey Graham kutoka South Carolina amewaambia wanahabari kwamba yeye haoni kama hilo ni wazo zuri.

    Upigaji kura wa Taifa umeonesha kwamba Trump anaachwa nyuma na mpinzani wake wa Democratic Joe Biden kwa asilimia 50.1 huku Trump akiwa na asilimia 41.9.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako