• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mchezaji mwingine wa Timu ya taifa ya wanawake ya Kenya Harambee Starlets atafuta bahati yake Ulaya

    (GMT+08:00) 2020-07-31 17:45:29

    Mshambuliaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Kenya Harambee Starlets Lilly Awuor amesema ana hamasa kubwa kwenye kutimiza ndoto yake ya kucheza katika Frauen-Bundesliga, yaani ligi kuu ya wanawake ya Ujerumani. Bi Awuor, ambaye hivi karibuni amejiunga na timu ya Ujerumani, Borrusia Pankow kwa mkataba wa miaka miwili, amesema hatua hiyo ni mwanzo tu wa safari yake ya kikazi nchini Ujerumani. Amesema yeye bado ni kijana kutoka Kenya na kwa hivyo ni ndoto yake kubwa ni kucheza timu nzuri barani Ulaya. Borrusia Pankow ilimaliza ya tatu msimu uliopita na sasa ina hamu ya kupanda daraja. Nyota huyo ilianza kuonekana alipocheza katika Ligi ya Wanawake Tanzania Bara alipoichezea timu ya Kigoma Sisters kabla ya kuhamia Sweden ambapo alijiunga na klabu ya Hammarby. Lilly ni mmoja a wachezaji wa Kenya wanaotafuta kuendeleza vipaji vyao barani Ulaya mmoja wao akiwa ni Ruth Ingosi ambaye anatarajia kufanya makubwa katika kikosi cha FC Lakatamia nchini Cyprus.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako