• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona barani Afrika yakaribia laki 9

  (GMT+08:00) 2020-07-31 19:05:50

  Takwimu kutoka Kituo cha udhibiti na kinga ya magonjwa cha Afrika (Africa CDC) jana zilionyesha kuwa, idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona barani Afrika imefikia 893,365 na idadi ya watu waliokufa kutokana na ugonjwa huo imefikia 18,881, na watu 541,959 wamepona.

  Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe tarehe 30 aliwaambia waandishi wa habari kuwa, majibu ya kipimo cha virusi vya Corona cha waziri wa kilimo Bw. Perrance Shiri aliyefariki tarehe 29 yalionesha kuwa aliambukizwa virusi hivyo.

  Waziri wa kazi wa Zanzibar Bw. Maudline Castico tarehe 30 alisema tangu virusi vya Corona vilipuke, watu zaidi ya 5,000 waliofanya kazi kwenye sekta ya utalii Zanzibar wamepoteza kazi.

  Serikali ya Rwanda tarehe 29 katika mkutano wa baraza la mawaziri ilisisitiza kuwa inapaswa kuimarisha ufahamu na hatua za kinga na udhibiti dhidi ya COVID-19, na kutangaza kuwa Rwanda itafungua usafiri wa ndege za abiria kuanzia tarehe 1 mwezi Agosti, lakini mipaka yake ya ardhini itaendelea kufungwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako