• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uchumi wa Marekani waporomoka kwa asilimia 32.9 katika robo ya pili ya mwaka huu

  (GMT+08:00) 2020-07-31 19:06:28

  Wizara ya biashara ya Marekani tarehe 30 ilitangaza makadirio yake ya kwanza kuhusu ukuaji wa uchumi, ikisema kuwa kutokana na kusitishwa kwa shughuli za kiuchumi na matumizi kunakosababishwa na janga la virusi vya Corona, Pato la Ndani la Marekani liliporomoka kwa asilimia 32.9 katika robo ya pili ya mwaka huu, kiwango ambacho ni kikubwa zaidi kushuhudiwa tangu mwaka 1947.

  Takwimu zinaonesha kuwa katika robo ya pili ya mwaka huu, matumizi binafsi yanayochangia asilimia 70 ya uchumi wa Marekani, yalipungua kwa asilimia 34.6. Matumizi ya huduma yaliyoathiriwa vibaya kutokana na mlipuko wa COVID-19 yalishuka kwa asilimia 43.5.

  Ili kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona, Marekani ilianza kutekeleza amri ya kukaa nyumbani na kufunga sehemu zisizo na ulazima kuanzia mwezi Machi, na kusababisha mporomoko mkubwa zaidi wa uchumi ambao haujawahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako