• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Homa ya mafua ya ndege yaripotiwa jimboni Victoria, Australia

    (GMT+08:00) 2020-08-03 08:43:42

    Maambukizi ya homa ya mafua ya ndege aina ya H7N7 yameripotiwa hivi karibuni kwenye shamba moja katika jimbo la Victoria nchini Australia. Hivi sasa shamba hilo na maeneo ya karibu yenye umbali wa kilomita tano yamefungwa, na ndege wote waliofugwa wamechinjwa. Kwa mujibu wa wizara ya afya ya jimbo hilo, hadi sasa bado hakuna watu walioripotiwa kuambukizwa homa hiyo, na idara za afya zinafuatilia hali ya afya ya wafanyakazi wa shamba hilo na watu waliowahi kuwa karibu na ndege walioambukizwa.

    Victoria pia ni jimbo linaloathiriwa vibaya zaidi na mlipuko wa virusi vya Corona nchini Australia, na jana usiku lilitangaza hali ya janga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako