• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chombo cha Uchunguzi wa sayari ya Mars cha China charekebisha robiti yake kwa mara ya kwanza

    (GMT+08:00) 2020-08-03 10:00:53

    Chombo cha Uchunguzi wa Sayari ya Mars cha China Tianwen No.1 kimefanikiwa kurekebisha obiti yake kwa mara ya kwanza Jumapili asubuhi.

    Habari zilizotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga za Juu ya China (CNSA) zinasema, chombo hicho kilirekebisha obiti yake baada ya injini yake aina ya 3000N kufanya kazi kwa sekunde 20, na kuendelea kuelekea kwenye sayari ya Mars, na mifumo yote ya chombo hicho ilikuwa katika hali nzuri.

    Kabla ya marekebisho hayo chombo hicho kilikuwa kimesafiri kwa zaidi ya saa 230, na kimekuwa umbali wa kilomita milioni tatu kutoka sayari ya Dunia.

    Marekebisho hayo pia yamejaribu utendaji wa injini ya 3000N. CNSA imesema chombo cha Tianwen No. 1 kitarekebisha obiti yake mara kadhaa katika safari ya kwenda Mars itakayochukua muda wa zaidi ya miezi sita.

    China ilirusha chombo hicho cha utafiti wa sayari ya Mars tarehe 23 Julai, ambacho kinatarajiwa kuzunguka, kutua na kutembea kwenye sayari hiyo, ikiwa ni hatua ya kwanza ya utafiti wa sayari za mfumo wa Jua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako