• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Victor Wanyama atawazwa mchezaji bora wa mtanange wa MLS

    (GMT+08:00) 2020-08-03 15:32:34

    Nahodha wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars, Victor Wanyama anaonekana kuwa amerejesha makali yake miezi michache baada ya kuhamia Major League Soccer. Wanyama alikatiza mkataba wake na Tottenham Februari mwaka huu na kujiunga na Montreal Impact, na kumaliza masaibu yaliyokuwa yanamwandama katika klabu hiyo ya London kaskazini. Hata hivyo, Mkenya huyo sasa anaoneka kuwa kwenye kilele cha taaluma yake, hii ni baada ya mchezaji huyo kutawazwa mchezaji bora wa mtanange wa MLS. Wanyama alituzwa taji hilo maridadi licha ya kuondolea kutoka kwenye mashindano hayo katika raundi ya mtoano. Alikuwa mchezaji wa timu ya kwanza katika mechi zote za Montreal Impact za Kundi C hadi walipofuzu. Alitajwa kama mchezaji bora wa mechi hiyo wakati kikosi chake kinachoongozwa na Thierry Henry kilipata ushindi dhidi ya DC United na kufaulu kwa raundi ya mtoano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako