• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Simba SC yatwaa taji la Shirikisho msimu wa 2019-2020

    (GMT+08:00) 2020-08-03 15:33:25

    Mabingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Simba SC hatimaye wametwaa taji la Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC) msimu wa 2019-2020 baada ya ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Namungo FC katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa. Katika mchezo huo uliokuwa wa vuta ni kuvute dakika zote 90, Simba SC ilianza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata mabao hayo dakika ya 28 kupitia kwa mshambuliaji wake, Luis Jose Miquissone wakati bao la pili likifungwa na nahodha John Raphael Bocco dakika ya 39, bao la Namungo likifungwa na Beki wa pembeni, Edward Charles Manyama dakika ya 56. Katika Michuano hiyo ya ASFC, Kiungo Mshambuliaji wa Simba SC, Cloutous Chama ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Michuano hiyo. Simba SC msimu huu wa 2019-2020 imejikusanyia mataji matatu ya Ngao ya Hisani, Ligi Kuu Soka Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho (ASFC).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako