• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDI: OBFT yawapa mchongo mabondia

    (GMT+08:00) 2020-08-03 15:34:04

    Shirikisho la Ngumi za Wazi Tanzania (OBFT) limetoa nafasi kwa mabondia wenye sifa kushiriki mashindano ya wazi ya taifa yanayoanza leo Agosti 3 jijini Dar es Salaam. Rais wa Shirikisho hilo Mutta Lwakatare amesema, mashindano hayo ni mwanzo wa maandalizi ya kuunda timu ya taifa itakayoandaliwa kwa ajili ya mashindano ya kimataifa ikiwemo michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwakani. Amesema mikoa ya Njombe, Iringa, Mwanza, Morogoro, Pwani, Singida Mbeya na wenyeji Dar es Salaam imethibitisha kushiriki mashindano hayo yanayofanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Parkers, Kawe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako