• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wasema uchaguzi wa Marekani utafanyika Novemba kama ilivyopangwa

    (GMT+08:00) 2020-08-03 16:14:15

    Maofisa kutoka Ikulu ya Marekani wamesema, uchaguzi wa rais nchini humo utafanyika Novemba 3 kama ilivyopangwa, baada ya rais Donald Trump awali kutoa uwezekano wa kuahirishwa kwa uchaguzi huo.

    Mkuu wa Utumishi katika Ikulu ya Marekani Mark Meadows amesema hayo jana katika kipindi cha televisheni ya CBC kinachoitwa Face the Nation.

    Kauli ya Meadows iliungwa mkono na mshauri wa kampeni ya urais Jason Miller, ambaye alikiambia kituo cha televisheni cha Fox News kuwa uchaguzi utafanyika Novemba 3 na rais Trump anataka uchaguzi ufanyike katika tarehe hiyo.

    Alhamis iliyopita, rais Trump alieleza uwezekano wa kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais mwezi Novemba, akidai kuwa upigaji kura kwa njia ya posta ni udanganyifu na si wa kuaminika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako