• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya imejitahidi kudhibiti nzige lakini tishio bado lipo Afrika Mashariki:FAO

    (GMT+08:00) 2020-08-03 16:52:39
    Kenya imepiga hatua kubwa katika kudhibiti nzige wa jangwani ambao walivamia eneo la Afrika Mashariki mapema na kwingineko mwezi February na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazao ilioweka maisha ya mamilioni ya watu njiapanda hasa katika suala la uhakika wa chakula. Limesema shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO.

    Kwa mujibu wa taarifa ya FAO iliyotolewa wiki jana mjini Roma Italia, kati ya nchi 29 zilizokumbwa na nzige hao waharibufu, 26 zimefanikiwa kuwadhibiti lakini tatu bado zinapambana zikiwemo Kenya , Somalia na Ethiopia.

    Hata hivyo shirika hilo linatumai kwamba katika siku chache zijazo zitasalia nchi mbili na ndani ya wiki tatu Kenya na Ethiopia nazo zitajikomboa kwa kiasi kikubwa.

    Pamoja na mafanikio hayo Cyril Ferrand kiongozi wa FAO wa masuala ya mnepo katika eneo la Afrika Mashariki ameonya kwamba nchi hizo zinapaswa kujitahidi kwani tishio la kuzuka upya mzunguko mwingine wa nzige wa jangwani mwishoni mwa mwaka huu bado lipo.

    Ameongeza kuwa miongoni mwa nchi zote 29 zilizokumbwa na nzige wa jangwani mwaka huu Kenya ndio iliyoathirika vibaya zaidi baada ya kutoshuhudia nzige kwa miaka 70 ikifuatiwa na Ethiopia, Somalia na Sudan Kusini. Juhudi kubwa za FAO kwa kushirikiana na wizara husika za kilimo na chakula katika nchi zilizoathirika zimefanikisha kuokoa karibu ekari laki sita Afrika Mashariki na kuua nzige bilioni 400 hatua iliyozuia uharibifu mkubwa wa mazao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako