• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu za madaktari kutoka China bara zatoa misaada kwa Hongkong kukabiliana na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-08-03 16:58:23
    Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong nchini China unakabiliwa na mlipuko wa virusi vya Corona, ambapo hadi kufikia jana tarehe 2, kesi mpya zilizothibitishwa kwa siku zilifikia 115, na idadi hiyo inazidi mia moja kwa siku 12 mfululizo.

    Kutokana na ombi la serikali ya Hong kong, serikali kuu ya China imetuma timu za madaktari kutoka China bara kwenda Hongkong kuisaidia kupambana na virusi hivyo.

    Timu ya kwanza ya upimaji wa virusi vya Corona imewasili jana huko Hongkong na kupokelewa vizuri. Mshauri wa Bodi ya Hospitali ya Renji ya Hongkong Bw. Wu Zhibin amesema, hivi sasa uwezo wa Hongkong wa kupima virusi vya Corona ni kwa watu elfu nane hadi tisa kwa siku, ambayo haiwezi kukidhi mahitaji ya mkoa huo, na timu kutoka China bara zinaziba pengo la Hongkong katika sekta hiyo.

    Wakazi wa mkoa wa Hongkong pia wanaona kuwa, timu za madaktari wa China bara kutoa misaada kwa Hongkong kunaonesha uungaji mkono wa serikali kuu kwa raia wa Hongkong na kuweza kupunguza kwa ufanisi matatizo ya kosefu wa vifaa vya matibabu na wahudumu wa afya yanayoikumba Hongkong.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako