• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyama viwili vya Marekani bado havijafikia makubaliano kuhusu msaada mpya wa fedha nchini humo

    (GMT+08:00) 2020-08-03 17:16:51

    Mpango wa misaada wenye thamani ya dola za Marekani trilioni 2 uliopitishwa na Bunge la Marekani mwishoni mwa Machi ili kusaidia kukabiliana na athari ya virusi vya Corona (COVID-19) umemalizika mwishoni mwa mwezi uliopita.

    Katika mpango huo, malipo ya dola 600 yalitolewa na serikali kwa wiki kwa watu waliopoteza ajira kutokana na athari ya virusi hivyo.

    Lakini, mpaka tarehe mosi, mwezi huu, chama cha Republican na chama cha Democrats bado havijafikia makubaliano kuhusu msaada mpya wa kifedha.

    Wanauchumi wameonya kuwa, kama mpango mpya hautatolewa kwa wakati, uchumi wa Marekani ulioshuka utaendelea kupata hasara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako