• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Eymael aigomea adhabu ya TFF asema haijafuata sharia

    (GMT+08:00) 2020-08-07 15:31:58

    Aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya soka ya Yanga, Luc Eymael amesema kuwa hakubaliani na adhabu iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ya kumfungia miaka miwili na kumtaka alipe faini ya Shilingi Milioni 8 kutokana na adhabu hiyo kukiuka taratibu za kisheria ikiwamo kutotoa nafasi ya yeye kujitetea. Eymael hivi karibuni aliingia matatani baada ya kutoa kauli zilizotafsiriwa kuwa ni za kibaguzi baada ya mchezo wao dhidi ya Lipuli. Akizungumza kutokea nchini Ubelgiji, kocha Luc alisema hajapokea taarifa rasmi kutoka TFF kuhusu kufungiwa kwake, bali anaona taarifa hizo kwenye mitandao ya kijamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako