Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Tedros Ghebreyesus amesema, kukabiliana na mlipuko endelevu wa COVID-19 kunahitaji ushirikiano na jitihada za pamoja za jumuiya ya kimataifa, na anatarajia Marekani itafikiria tena uamuzi wake wa kujitoa kwenye Shirika hilo.
Dr. Ghebreyesus amesema, WHO inakaribisha mapendekezo ya maboresho yoyote, endapo Marekani inaona kuna masuala yanayohitaji kufanyiwa marekebisho katika Shirika hilo, na haina haja ya kutumia njia ya kujitoa.
Dr. Ghebreyesus amesema, Marekani bado inaendelea kushiriki kwenye mikutano ya Shirika hilo na kudumisha mawasiliano, na anatarajia uhusiano kati ya pande hizo mbili urudishe kwenye hali ya kawaida.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |