• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyombo vya habari vya Marekani vyapingana kuhusu utendaji wa serikali katika kukabiliana na COVID-19 na maandamano

    (GMT+08:00) 2020-08-07 16:44:35

    Ikiwa imesalia miezi mitatu kabla ya uchaguzi wa urais nchini Marekani, vyombo vya habari nchini humo na wananchi vina mjadala mkali juu ya nani atakayeiongoza nchi hiyo katika wakati ambao biashara nyingi nchini humo zimeathiriwa vikali baada ya kufungwa kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona.

    Baadhi ya vyombo vya habari nchini Marekani kama CNN, The Washington Post na The New York Times vimekosoa hatua zilizochukuliwa na serikali ya Marekani katika kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona na maandamano yaliyotokana na ubaguzi wa rangi, huku vyombo vingine vya habari kama FOX News vikipongeza juhudi za serikali hiyo katika kukabiliana na janga hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako