• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatumai Marekani itashinda mapema mapambano dhidi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-08-07 18:36:30

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema, China inatumaini kuwa Marekani itashinda mapema mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona, pia inatarajia baadhi ya wanasiasa wa Marekani wataacha vitendo vya kuhamishia uwajibikaji wake kwa China.

    Kauli hiyo imekuja baada ya balozi wa Marekani nchini China Bw. Terry Edward Branstad aliyefika mjini Shanghai jana, na kusema kuwa vifaa vya matibabu vilivyotolewa na China kwa Marekani vimeokoa maisha ya watu wengi, na kueleza kuwa anatarajia kuhimiza mawasiliano na ushirikiano na China, na kukabiliana na athari mbaya inayotokana na maambukizi ya virusi.

    Akizungumzia kauli ya Bw. Branstad, Bw. Wang amesisitiza kuwa magonjwa ya kuambukiza hayajali mipaka ya nchi na makabila, na ni adui wa pamoja kwa binadamu wote, na kwamba mshikamano na ushirikiano ni silaha zenye nguvu zaidi, na kuokoa maisha ni jukumu linalohitajika zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako