• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu zaidi ya laki moja wakosa makazi nchini Sudan Kusini kutokana na mafuriko

    (GMT+08:00) 2020-08-07 19:26:21

    Watu 150,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mafuriko yaliyotokea mashariki mwa mkoa wa Jonglei nchini Sudan Kusini.

    Mkurugenzi wa Tume ya Misaada na Ukarabati nchini humo Gabriel Deng Ajak amesema, maelfu ya watu wamekosa makazi katika sehemu nyingi za mkoa huo, ambao pia umeshuhudia mapigano ya kikabila tangu mwezi Julai.

    Amesema kiwango cha maji kimeongezeka kwa mita 1.5 kutokana na mvua kubwa zilizonyesha tangu mwezi Julai, na kuongeza kuwa, mapigano ya kikabila yaliyoanza mwezi huo Julai yameathiri watu laki nne katika mkoa huo kabla ya mafuriko hayo kutokea. Ametoa wito kwa serikali kuu na mashirika ya kimataifa kusaidia wananchi wa Sudan Kusini kukabiliana na changamoto hizo.

    Mwaka jana, mashirika ya Umoja wa Mataifa yalikadiria kuwa watu laki tisa walipoteza makazi yao kutokana na mafuriko katika mikoa ya Jonglei, Pibor na Eastern Equatoria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako