• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaweka mtandao wa uchukuzi na ugavi ili kupunguza gharama za biashara

    (GMT+08:00) 2020-08-07 20:43:57

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameanzisha mfumo wa usimamizi, uratibu na mwingiliano wa bandari, reli na huduma za umma za mafuta chini ya Mtandao wa Uchukuzi na Ugavi wa Kenya, (KTLN).

    Katika waraka maalum uliotolewa jijini Nairobi hii leo, rais Kenyatta amesema mtandao huo unazikutanisha Mamlaka ya Bandari (KPA), Shirika la Reli la Kenya (KRC) na Shirika la Mafuta la nchi hiyo (KPC) chini ya uratibu wa Shirikisho la Maendeleo ya Viwanda na Biashara (ICDC).

    Rais Kenyatta amesema, KYLN italeta usawa katika umakini na maingiliano ya taasisi hizo nne za taifa ili kutimiza ajenda ya kimkakati ya Kenya ya kuwa kitovu cha ugavi katika kanda hiyo.

    Pia amesema, utaratibu huo mpya unatarajiwa kusaidia kushuka kwa gharama za kufanya biashara nchini humo kupitia upatikanaji wa miundombinu ya reli, bandari na mafuta kwa gharama nafuu, na ndani ya viwango vinavyohitajika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako