• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wazindua mradi wa kuzisaidia biashara barani Afrika

    (GMT+08:00) 2020-08-12 08:57:33

    Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika (AUDA-NEPAD) jana limezindua mradi utakaozisaidia kampuni changa, ndogo na za ukubwa wa kati (MSMEs) barani humo, kurekebisha shughuli zao katika mazingira ya janga la COVID-19.

    Shirika hilo limeshrikiana na kundi la Ecobank, na kuanzisha Chuo cha MSMEs, ambacho kitatoa mafunzo ya utendaji na rasilimali kuhusu fursa za ufadhili kwenye nchi mbalimbali, jinsi ya kujenga biashara za kidijitali na jinsi ya kurekebisha biashara katika mazingira ya Janga kubwa la COVID-19.

    Chuo hicho pia kitatoa habari za masoko, na washauri wengi wenye uzoefu tofauti, wakati huo huo, kitazisaidia kampuni hizo kupata fursa za ufadhili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako