• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa ngazi ya juu wa China na Afrika watoa wito wa kuimarisha ushirikiano dhidi ya janga la COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-08-12 09:51:19

    Wataalam wa ngazi ya juu wa Afrika na China wametoa wito wa kuimarisha zaidi uhusiano kati ya pande hizo mbili katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona barani Afrika.

    Katika mkutano huo uliofanyika kwa njia ya video jana, naibu mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Kwei Quartey amesisitiza umuhimu wa mshikamano wa China na Afrika katika kupambana na janga hilo. Amesema Kamati yake inaishukuru China kwa kuendelea kuunga mkono na ahadi yake ya kuungana na Afrika katika kudhibiti na kuzuia kuenea kwa magonjwa barani humo, hususan janga la virusi vya Corona.

    Balozi wa China katika Umoja wa Afrika, Liu Yuzi pia amesisitiza kuwa katika wakati mgumu ambao China ilikuwa ikipambana na janga hilo, Umoja wa Afrika na nchi za Afrika ziliiunga mkono na kutoa misaada ya fedha na vifaa kwa China. Amesema baada ya mlipuko kutokea barani Afrika, China ilichukua nafasi ya uongozi na kutoa msaada na kusimama pamoja na watu wa Afrika kukabiliana na janga hilo kwa kupeleka vifaa tiba na wataalam kwa nchi za Afrika na Umoja wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako